Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati aliyeketi) na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (kushoto aliyeketi), wakisaini Hati za Mkataba (Exchange of Notes) kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Japan, wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, ambapo katika hafla hio Mhe. Dkt. Nchemba alisaini Hati ya Mkataba mwingine wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).




