Mwenyekiti
wa tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs
Mwambegele akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji
wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya
Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri
yaliyoanza leo tarehe 17 hadi 18 Januari, 2025 Mkoani Mtwara ambapo
amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili
viweze kutumika katika maeneo mengine nchini pamoja na kuzangitia
mafunzo hayo ili wakafanikishe zoezi hilo muhimu.
Zoezi
la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani humo linataraji
kuanza Januari 28,2025 na kufikia tamati Februari 03,2025 huku vituo
vikitaraji kufunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:jioni kwa
siku zote saba.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi, Ndg. Kailima, R. K akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mkaguzi
Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Fredrick Mwanamboje akiwasilisha
mada ya uraia kwa watendaji wa uboreshaji mkoa wa Mtwara wakati wa
mafunzo ya siku mbili ya watendaji hao ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani huo. Watendaji hao ni pamoja
na Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa
waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi
na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mst)
Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 17 Januari, 2025 amefungua mafunzo ya
watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya
mkoa, mkoani Lindi ambapo amewataka watendaji hao kutunza vifaa vya
uboreshaji wa Daftari na kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume
wakati wote wa utendaji wao.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huo
ambao utafanyika sambamba na Mkoa wa Mtwara na mkoani Ruvuma kwenye
Halmashauri za Wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru kuanzia tarehe 28
Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari, 2025 na ambapo vituo vitakuwa
vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Na
Waandishi wetu,Mafunzo kwa Watendaji wa uchaguzi katika mikoa ya
Mtwara, Lindi na Ruvuma katika halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo
na Tunduru ikiwa ni mzunguko wa 10 wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura yamefunguliwa leo mkoani Mtwara na Mwenyekiti wa Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jacobs
Mwambegele.
Mafunzo kama hayo pia yamefunguliwa katika mikoa ya
Lindi na Ruvuma ambapo mkoani Lindi mafunzo hayo yamefunguliwa na Makamu
Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk
na mkoani Ruvuma, mafunzo hayo yamefunguliwa na Mjumbe wa Tume Mhe.
Magdalena Rwebangira.
Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa
Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa
Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi
na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 17 hadi 18
Januari, 2025 Mkoani Mtwara Mhe. Jaji Mwambegele amewataka watendaji hao
kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili viweze kutumika katika
maeneo mengine nchini.
Amesema ni muhimu kutekeleza majukumu
yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya
uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama
kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya
uandikishaji nchini.
Mkoani Lindi, Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk amewaambia
watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari katika mikoa hiyo,
mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya
kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika
zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo
husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Amewaambia
watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama
vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura
jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia
mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza
kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Hata hivyo Mhe. Jaji
Mbarouk amesisitiza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji
wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Mjumbe wa Tume Huru
ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Rwebangira ambaye amefungua mafunzo
hayo kwa watendaji wa uboreshaji katika mkoa wa Ruvuma ameeleza kuwa
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea umahiri watendaji hao ili waweze
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao
watatoa mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na
Waandishi Wasaidizi ambao ndio watakaohusika na uandikishaji wa wapiga
kura vituoni.
Ameongeza kuwa Maafisa TEHAMA nao watapatiwa
mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za
kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la
uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Mafunzo hayo ambayo
yanafanyika kwa muda wa siku mbili ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa ya Mtwara, Lindi na
Ruvuma katika halmashauri za wilaya ya Madaba, Namtumbo na Tunduru ambao
utafanyika kuanzia tarehe 28 Januari, 2025 hadi tarehe 03 Februari,
2025.
Mratibu
wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa waandikishaji
wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa
TEHAMA wa Halmashauri wamekula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya
siasa na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa
Mtwara, Mhe. Lucas Jang’andu ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuanza kwa
mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa katika
Mkoa wa Mtwara.