Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, akikabidhi kwa Nahodha wa timu ya Wafanyabiashara Kariakoo, Shafii Salimu, kombe baada ya kuifunga timu ya TRA, katika michuano ya bonanza la Siku ya mlipakodi, viwanja vya Michezo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam, jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
Wafanyabiashara wa Kariakoo na watumishi wa TRA, wakichuana katika mchezo wa kukimbia na magunia katika viwanja vya Michezo Jakaya Kikwete, jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, akikagua timu ya Wafanyabiashara Kariakoo na TRA, katika bonanza la michezo la kuazimisha wiki ya mlipakodi, viwanja vya Michezo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam, jana. Mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.Timu hizo zilitoka suluhu.