Meneja Utawala wa hoteli ya kitalii ya PALACE, Joseph Mremi akizungumza katika hafla hiyo mkoani Arusha.


………….
Happy Lazaro,Arusha .
WADAU wa Sekta ya Utalii wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuanzisha Royal Tour ambayo imekuwa na matokeo Chanya katika kukuza utalii mkoani Arusha kupitia biashara ya Mahoteli.
Hayo yameelezwa mkoani Arusha na Meneja Utawala wa hoteli ya kitalii ya PALACE, Joseph Mremi , katika hafla ya kupongezana kwa menejimenti ya hoteli hiyo pamoja na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kukuza utalii Arusha, hafla iliyofanyika katika hoteli hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
“lengo kuu la hafla hii ni kumuunga Mkono Rais wetu Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza utalii kupitia Royal Tour ambayo imekuwa na tija kubwa kwetu kama wadau wa Utalii”amesema Meneja huyo.
Amesema hafla hiyo pia ililenga kuwakutanisha na wadau wengine wa utalii ambao wamekuwa msaada mkubwa katika ustawi wa hoteli hiyo katika kujenga mahusiano ya kibiashara tangu kuanzishwa kwake miaka kumi na tano iliyopita.
“lengo lingine lililotukutanisha hapa ni kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa utalii katika kukuza biashara zetu na kuitangaza Arusha”amefafanua .
Mremi amewashukuru wadau wa utalii waliojumuika katika hafla hiyo iliyoenda sanjari la kuwashukuru wafanyakazi wa hotel hiyo kwa ushirikiano wao na kuwapa zawadi .
Aidha ametaja huduma mbalimbali zinazotolewa katika hoteli hiyo kuwa ni pamoja na huduma za Mikutano,Chakula,Mazoezi ,Sauna na Ateam Bath bure,kufua nguo kwa wageni kutoka nje ya hotel kwa gharama ndogo.
Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali wa utalii mkoani Arusha kuitumia hoteli hiyo kwa ajili ya huduma mbalimbali ili kuunga mkono sekta hiyo.