TAASISI,Makampuni na Mashirika yanayowezesha Vifaa tiba Kwa Watu Wenye Ulemavu Wameshauriwa Kufanya Uchunguzi wa Vifaa tiba Sahihi vya Kuwapatia Walemavu ili Kuwanusuru na changamoto mbalimbali ikiwemo Magonjwa ya Vidonda mgandamizo.
Akizungumza wakati wa Semina ya Vifaa tiba sahihi Kwa Walemavu iliyoandaliwa na Taasisi ya Kubuni na Kutengeneza Vifaa saidizi Kyaro Assesive Tech Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Colman Ndetembea amesema Wadau mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele Kuhakikisha Walemavu wanapata Vitimwendo Kufanya mijengeo sehemu moja Kwenda nyengine lakini ni muhumu kufahamu vitimwendo sahihi kwa kuangalia umri wa Mtu,aina ya Ulemavu wake pamoja na eneo ambalo anaishi ili viweze kukidhi Mahitaji kwa haraka na nafuu.
Hata hivyo Colman ameongeza zaidi Kuwa Taasisi yake ya Kyaro imekuwa watoaji huduma za Vifaa tiba hasa Vitimwendo Kwa kuangalia kwanza Matakwa ya mteja na ubora wa Kiti hicho ili Kiweze kumfaa kwa Miaka mingi kikiwa kwenye ubora wake .
Kwa Upande wake Mkufunzi wa Semina hiyo Kutoka Hospitali ya Ccbrt Jijini Dar es Salaam Neophita Lukiringi ameongeza kuwa Kumpatia Mlemavu Kitimwendo sio sahihi ni Kusababisha Magonjwa mbalimbali ikiwemo Kutokwa na Vidonda katika Uti wa Mgongo na Kusababisha maradhi mengine ya kudumu kutoka na kupitia mateso kwenye Kiti ambacho sio sahihi kwake.
” Unapompatia Mlemavu Kitimwendo ambacho sio sahihi unamsababishia Magonjwa ikiwemo Vidonda mgandamizo katika Uti wake wa Mgongo,ufupisho wa misuli hasa kwa wale ambao Kitimwendo ni kirefu kuliko kimo chake, hata hivyo Mlemavu anakosa ufanisi na uhuru wa kujiamini mbele ya Jamii inayomzunguka.”
Hata hivyo amesema Wadau hao Wanaotoa msaada wa Vifaa tiba hivyo ni muhimu zaidi Kuwasiliana na Serikali za Mitaa,Nyumba za Ibada,Ustawi wa Jamii ili kuweza kupata idadi ya Wahitaji na umri wa wahitaji pamoja na aina ya Vitimwendo kwa Mahitaji ya Muhusika.
Lukiringi ametoa rai Kwa Wadau wanaosaidia Vitimwendo Kwa Watu wenye Ulemavu Kufanya utafiti Viti sahihi kabla ya kuwagawia ili Viweze Kuwa msaada kwao na Kuweza Kufanya mijengeo sehemu moja kwenda nyingine.
Nae Mmoja wa Nufaika wa Semina hiyo Ramadhan Juma amesema ili tuweze Kupunguza kadhia ya Magonjwa mapya ikiwemo vidonda mgandamizo, Kwa Msaada wa Vifaa tiba hivyo lazima Wanaotoa misaada hiyo wapewe Semina elekezi ya namna Vifaa tiba gani ni sahihi kwao kutokana na Mazingira waliopo na aina ya Ulemavu. Mkufunzi wa Semina ya Vifaa Tiba sahihi Kwa Walemavu kutoka Hospitali ya Ccbrt Jijini Dar es Salaam Neophita Lukiringi akiendesha Mada Kwa Wanahabari,Wakuu wa Taasisi na Vyama ya Walemavu
Picha ya Pamoja Kati ya Wakufunzi wa Semina ya Vifaa tiba pamoja na Wanahabari na Wadau wa Elimu Kwa watu wenye Ulemavu nchini iliyofanyika Katika Hospitali ya Ccbrt Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kubuni na Kutengeneza Vifaa tiba Kyaro Assesive Tech Colman Ndetembea akifafanua zaidi Vifaatiba mbalimbali ikiwemo Vitimwendo,Kifaa cha Masikio Kwa Viziwi katika Semina ya Vifaa tiba iliyofanyika katika hospitali ya Ccbrt Jijini Dar es Salaam