NA BELINDA JOSEPH, RUVUMA.
Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Ruvuma, limewataka wananchi kukubaliana na bei elekezi za umeme bila kuwa na malalamiko kwani jukumu zima la bei halipo chini ya Shirika hilo isipokuwa kwa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji yaani EWURA hivyo hakuna namna yoyote ya wao kuweza kubadili bei hizo zilizopangwa.
Ufafanuzi huo umetolewa na Afisa uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ruvuma Alan Njiro, kufuatia ombi la wakazi wa Kata ya Mletele Manispaa ya Songea kutoa ombi kwa Shirika hilo kuweza kupunguza bei ya kuunganisha huduma hiyo kwa wateja wapya kwa shilingi elfu 27 badala ya bei elekezi ya laki tatu na elfu 20 kutokana na hali zao za kiuchumi, ambapo amewataka kufuata taratibu zilizopo kwani wao sio wanaopanga bei hizo isipokuwa EWURA.
Amesema kuwa hadi hivi sasa tayari shirika limekamilisha ufungaji wa Transfoma jukumu lililobaki ni kwao wananchi kuanza kufanya maombi ya huduma hiyo kwani ni bure na Mara baada ya maombi hayo kukamilika ndani ya siku nne hadi saba mteja akilipia atakuwa amepata huduma ya umeme.
Kwa upande wa Afisa Msaidizi wa huduma kwa wateja kutoka TANESCO Ruvuma Bi Emma Ulendo, amewataka wakazi wa Mletele kuchangamkia fursa ya kuomba maombi ya umeme ili waweze kunufaika na huduma hiyo kwa kuanzisha biashara mbalimbali hata thamani ya ardhi nayo itapanda.
Diwani wa Kata ya Mletele Maurice Lungu amempongeza Rais Sa
mia kufikisha mradi huo wa umeme ambao umegharimu zaidi ya Milioni 144 hadi kukamilika kwake, huku akiwataka wananchi kuendelea kuchangamkia fursa hiyo ili umeme uweze kuwanufaisha kwa kufungua viwanda vidogovidogo, saluni n.k, shughuli zitakazowaletea maendeleo.
Ziara ya Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja kutoka TANESCO mkoa wa Ruvuma Alan Njiro bado inaendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huu ikiwa lengo ni kutoa elimu ya matumizi sahihi ya umeme kwa wateja wapya wa Shirika hil