Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Mudrik Ramadhan Soraga amewataka vijana kutumia fursa ya tehama ili kuleta mageuzi ya kiuchumi katika nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Mkoa wa Mjini Magharib kuhusu Mkutano wa Tech and AI International Expo.
Amesema jambo hili ni sahihi ambalo linaendana na mpango mikakati wa Serikali katika kuleta mageuzi katika sekta ya tehama Nchini.
Aidha Waziri Soraga amesema kuna kila sababu ya kuweka matukio haya katika visiwa vyetu na kuiweka Zanzibar katika ramani ya Dunia kama ni kitivu cha tehama. Amefahamisha kuwa kumekuwa na juhudi mbali mbali ambazo Serikali imekuwa zikichukua pamoja na mipango iliyokuwa ikiratibiwa na Taasisi mbali mbali.
“Hakujawahi kuwa na Jukwaa (Forum) ambalo linaleta wadau wa tehama kutika nchi mbali mbali kukutana sehemu moja wakati mmoja na kujadiliana mikakati ambayo inahusu tehama na inavyoweza kuunga mkono maswala ya tehama”
Alisema Waziri Soraga. Hata hivyo ameipongeza Taasisi ya Afrika Business Inc kutoka Afrika ya Kusini kwa kuja na mpango ambao utaleta mafanikio nchini pamoja na kushirikiana na wadau mbali mbali watakaowezesha kuongeza thamani katika tukio hilo.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa katika Visiwa vya Zanzibar kumebahatika kuwa na vijana wengi ambao wamemaliza masomo ya Tehama ambao wamekosa muongozo mzuri hivyo kupitia ujio huu watapata fursa yakufanikisha malengo yao.
Nae Afisa mkuu wa masoko na mkakati kutoka Afrika Business Inc Ms Lebohang Noruwana Mkhize amesema mkutano huo utakuwa na takribani washiriki 1500 kutoka Zanzibar pamoja na wajasiriamali wadogowadogo kutoka Afrika kuja kujumuika kwa pamoja ili kujua jinsi ya kufanyabiashara kupitia tehama.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Unique Touch Company Edwin Robert George amesisitiza ushirikiano katika kulikamisha kwa wakati ili kuitangaza Zanzibar Kimataifa.
Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Afrika Business Inc ya South Afrika na Parem Solutions kutoka UK kupitia Taasisi ya Unique Touch ya Zanzibar ambao utafanyika Agost 22 – 23, 2025.




