Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Imeelezwa kwamba wananchi wengi wanaoenda kupata Matibabu ya Afya katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo na Mishipa ya fahamu (MOI) ni magonjwa yanayosababishwa na ajali za barabarani hasa kwa vijana katika matumizi ya vyombo vya moto.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Mhe. Balozi. Dkt. Mpoki Ulusubisiya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo.
Amesema magonjwa hayo yanafuatiwa na magonjwa yanayosaabishwa na umri mkubwa kwa sababu makadirio ya umri wa kuishi kwa sasa yamefikia umri wa miaka 60 (life expectance) na jinsi mtu anavyozidi kuwa mkubwa ndivyo afya yake inakuwa na changamoto zaidi kwenye moyo na mifupa.
Dkt, Mpoki amesema, “Ongezeko la watu katika matumizi ya usafiri (bodaboda) pikipiki limesababisha ongezeko la ajali za pikipiki linalosababishwa na kukosekana kwa umakini wa madereva wa vyombo hivyo vya moto.”
Aidha kutozingatia weledi wa kufuata sheria za barabarani wakati wa matumizi ya vyombo vya moto imesababisha wananchi wengi kupata ajali kwa kushindwa kujali usalama wao wenyewe na abiria wao.
“Tunahitaji kuongeza nguvu katika mafunzo ya matumizi ya vyombo vya moto kwa kujali usalama wa barabarani na polisi wakasimamia ukaguzi wa leseni na utoaji wa leseni,” alihimiza
“Sisi tutaendelea kujikita katika kutoa huduma bora za afya endelevu na za kisasa kwa wateja wetu na kuondoa adha ya wananchi kufuata huduma hizi nje ya nchi.
Licha ya kujikita katika kutoa tiba”
Dkt Mpoki amesema Taasisi ya (MUHAS) inaendelea kufundisha wataalam katika Magonjwa ya Mifupa, katika Upasuaji wa Migongo Mishipa ya Fahamu pamoja na Ubongo,
na inajihusisha na ufundishaji upasuaji katika chuo kinachohudumia Nchi za Mashariki Kati na Kusini Mwaafrika, ikiwa ni pamoja na fani za mifupa kwa ajili ya magonjwa ya watoto, Upasuaji Mgongo, Ubongo na Mishipa ya Fahamu Ubobezi katika mifupa.