FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi,
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF), utakaofanyika katika Manispaa ya Songea, mkoani
Ruvuma, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Aprili 2025.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari mjini Morogoro leo Februari 7, 2025, Mwenyekiti wa
TEF, Deodatus Balile, amesema mkutano huo utawakutanisha wanachama wote
wa TEF kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa jukwaa hilo.
Balile
ameongeza kuwa TEF itahakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki, ikiwa
ni sehemu muhimu ya taasisi na vyama kujifunza namna bora ya kuendesha
chaguzi za kidemokrasia.
Amefafanua kuwa uchaguzi huo unafanyika
kwa mujibu wa Ibara ya 7 na Ibara ndogo ya 8 ya Katiba ya TEF, ambapo
muda wa uongozi wa sasa unafikia tamati baada ya kutumikia kwa miaka
minne tangu mwaka 2021.
Katika uchaguzi huo, wanachama watawachagua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, pamoja na wajumbe saba wa Kamati Tendaji ya TEF.
Aidha
amesema fomu za kuomba nafasi za uongozi zitaanza kutolewa rasmi
Jumatatu, Machi 10, 2025, katika ofisi za TEF zilizopo Mtaa wa Mtendeni,
Kisutu, jijini Dar es Salaam huku mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu
ni Machi 24, 2025, ifikapo saa 10:00 jioni.
Wagombea wanatakiwa
kurejesha fomu zao wakiwa na picha moja ndogo (passport size), ambayo
itatumika kwenye karatasi za kura endapo watachaguliwa kuwania nafasi
wanazoomba.
Pia muda wa kuchukua na kurejesha fomu ni kuanzia saa
3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika siku za kazi pekee. “Fomu
hazitatolewa wala kupokelewa siku za Jumamosi, Jumapili, na sikukuu”.
Amesema Balile
Amesema Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti ada ya fomu ni shilingi 150,000, huku ada kwa nafasi za
wajumbe wa Kamati Tendaji ikiwa ni shilingi 100,000 huku akisisitiza
Kuwa ada hizi hazitarejeshwa endapo mgombea atabadili mawazo.
Uchaguzi
huo utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na Frank Sanga kama
Mwenyekiti, pamoja na wajumbe Angel Mang’enya na Rashid Kejo. Kamati hii
ina jukumu la kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa, ikiwa
ni pamoja na vigezo na sifa za wagombea.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni ‘Uchaguzi Huru na wa Haki.’.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi