Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki Kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva – Uswis kuanzia tarehe 10 – 14 Machi, 2025.
Katika vikao hivyo Wizara imeweza kuwasilisha taarifa za Nchi zinazohusu haki za watu wenye ualbino, haki za watu wenye ulemavu na haki za watoto hasa ukatili dhidi ya watoto.
Aidha, Wizara imeshiriki Mkutano ulioandaliwa na Latin America kwa lengo la kupitia Mfumo wa Uandaaji na Ufuatiliaji Taarifa za Haki za Binadamu kwenye Mikataba ambayo Nchi ya Tanzania imeridhia.