Na Diana Byera,Missenyi
Mamia ya Wananchi wa Kata Nsunga vijiji vya Byamtemba ,Igayaza ,na Ngando wilayani Missenyi wamejitokeza kwa wingi kuwasilisha kero kwa wataalamu wa kisheria, ambao wamekuja kusikiliza na kutatua changamotoo za kisheria kupitia kampeni ya huduma za kisheria ya Mama Samia
Hii ni siku ya kwanza kwa wilaya hiyo mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria iliyozinduliwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Damas Ndumbaro mkoani Kagera, ambayo itatekelezwa kuanzia tarehe 14 hadi 23 mwaka huu.
Mamia ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Igayaza kata ya Nsunga wakiwa na shauku ya kuwasilisha changamoto zao na wengi wamesema hii ni mara ya kwanza kushuhudia wananchi wakaifuatwa na timu ya mawakili na wanasheria kwenda kuwasikiliza na kuwapa Elimu ya kisheria tangu nchi imepata uhuru.
“Kama wananchi tumefurahishwa na tukio la mama Samia kuleta huduma za kisheria wengi hawana uzoefu hata wakitapeliwa wanajiuliza tutaenda kwa nani ,tutaanzia wapi ,uwepo wa huduma za kisheria katika vijiji vyetu ni mwanga tosha kuwa serikali inawajali wananchi wake ,Hili ni jambo kuwa na ni faraja kwa wananchi wa wilaya ya Missenyi na Tanzania kwa ujumla “Amesema Reondar Lucas kutoka Kijiji Cha Igayaza.
Mratibu wa kampeini ya huduma za kisheria ya mama Samia wilaya ya Missenyi Maximilian Fransis alisema kuwa zaidi ya wananchi 1,000 wamejitokeza kuja kupata Elimu ya kisheria katika viwanja vya Igayaza na walifika kabla ya saa 3 Asubuh.
Alisema lengo la wataalamu waliokija kutekeleza kampein hiyo ni kuhakikisha wanatoa Elimu ya uhakika kwa wananchi wa wilaya hiyo ili kuwasaidia kuokoa muda mwingi ambao wanatumia mahakamani badala ya kufanya Shughuli za kuzalishaji
Alisema kuwa malengo ni kutatua migogoro yote ya kisheria asilimia 75 kwa vijiji 30 vya wilaya ya Missenyi ambavyo vitatembelewa hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kwani gharama za Kuwahudumua kisheria zimelipwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassani.