JAJI Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, akipata maelezo kutoka mkuu wa Divisheni Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar Bakari Omar Ali, wakati alipotembelea banda la idara hiyo, akiwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba sheria utumishi na Utawala Bora Dkt.Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jumanne Sagini, wakati wa Uzinduzi wa Kampenzi ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA)
JAJI Mkuu wa Zanzibara Khamis Ramadhan Abdalla, akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, kampeni hiyo ilioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar na Kufanyika katika viwanja vya bustani ya Mwanamashungi Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba sheria Utumishi na Utawala Bora Dkt.Haroun Ali Suleiman, akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia, kampeni hiyo ilioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar na Kufanyika katika viwanja vya bustani ya Mwanamashungi Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA)
NAIBU Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jumanne Sagini, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia, kampeni hiyo ilioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar na Kufanyika katika viwanja vya bustani ya Mwanamashungi Wilaya ya Chake Chake.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadidi Rashid, akitoa salamu za mkoa huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, kampeni ilioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar na Kufanyika katika viwanja vya bustani ya Mwanamashungi Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA MARIYAM SALIM,
WATENDAJI kutoka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar na watendaji kutoka Wizara ya Katiba na sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakifuatilia kwa makini halfa ya Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, ilioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar na Kufanyika katika viwanja vya bustani ya Mwanamashungi Wilaya ya Chake Chake.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA)
……..
pengine kutokana na kutokuwa na uwezo hivyo kampeni hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa makundi hayo kuweza kupata haki zao kwa mujibu wa sheria,”alieleza Mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya mawakili Zanzibar Joseph Magaza alisema uzinduzi wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia sio tu kwamba ni usaidizi wa upatikanaji wa haki,Bali ni uthibitishi wa uwepo wa haki za binaadamu Tanzania.
Magaza aliwataka wananchi na wanasheria kuelewa kwamba msaada wa kisheria ni daraja kati haki zilizoandikwa na haki halisi kwani msaada wa kisheria si anasa bali ni haki kwa kupata haki zinazomstakia.
Alisema kila mwananchi bila ya kujali Itikadi na uwezo wake anapata haki ya Ulinzi na mali yake kwa mujibu wa sheria.
Alifahamisha kuwa Kampeni hiyo inalenga kuongeza uwelewa wa kutowa huduma na kuhakikisha hakuna anaebaki nyuma katika kupata usaidizi wa kisheria, ushauri na uwakilishi.
“Jumuiya ya mawakili Zanzibar inalojukumu kubwa na sio kwa wanachama wake tu bali kwa jamii mzima ya Zanzibar kwani majukumu yetu yamejikita katika kulinda utawala wa sheria na kutetea haki na kuhakikisha maadili na weledi katika taaluma ya sheria Zanzibar kama ilivyo ainishwa katika kifungu cha 4 cha sheria cha Jumuiya ya mawakili Zanzibar sheria namba 7 ya mwaka 2019”, alisema.
Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya mama Samia tayari imeshawafikia zaidi ya watu 36 788 wakiwemo wanaume 16992 na wanawake 19866 kwa Mikoa mitatu kwa Zanzibar.