Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns Ian Gorowa ameachana na kazi hiyo ya kufundisha mpira wa miguu alikojipatia umaarufu na kuwa muhubiri wa Injili.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cape Town Spurs mwenyewe miaka 53, amefichua kuwa sasa ni mchungaji wa wakati wote katika kanisa la Apostolic Faith Mission, na hana mpango wa kurejea kwenye soka.
Kazi ya mwisho ya Gorowa katika soka ilikuwa mwaka wa 2014 kama kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe, karibu muongo mmoja baada ya kuachana na Sundowns.
“Ndiyo, nimeachana na ukocha kama taaluma sitarudi ,Ninashinda roho sasa,Safari kama mchungaji imekuwa nzuri sana. Ninaifurahia inatimiza na kuimarisha roho ya mtu,” amesema Kocha huyo mstaafu.




