
Katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Pili Kikao cha Tisa, leo tarehe 6 Februari 2026 Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mheshimiwa Bakari Shingo amependekeza uwepo wa utaratibu wa kutaja hadharani Watumishi waliotumia mlango wa nyuma kujikopesha fedha za Almashauri na vikundi vilivyokopeshwa mikopo hiyo na kupotea bila kuirejesha.
Pendekezo hilo lililokuja kwa njia la swali dogo la nyiongeza lilijibiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Reuben Kwagilwa; na kuongezewa maelezo na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Riziki Shemdoe kwa kutoa mrejesho wa kikao cha Wizara hiyo na mabenki yaliyopewa dhamana ya kuendesha mchakato huo kwa niaba ya Serikali.






