WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara zinazoambatana na mikutano ya hadhara katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Ziara hizo zilizoanza tangu Februari 13, mwaka huu zimeonesha taswira ya uongozi unaoshuka kwa wananchi, kusikiliza na kuchukua hatua. Akiwa mkoani Tanga alikoanzia ziara, Waziri Mkuu ameonesha kwa vitendo kuwa uongozi si kukaa ofisini kusubiri





