Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amegiza Vyombo vya Uchunguzi kumpatia taarifa ya kina haraka kuhusu tukio baya la mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Ali Kibao na mengine ya namna hiyo haraka.
Rais Samia amesema “Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi, Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii”
“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao, natoa pole kwa Viongozi wa Chama hicho, Familia ya Mzee Kibao, Ndugu, Jamaa na Marafiki.
The post Rais Samia alizwa mauaji ya Mzee Ali Kibao wa Chadema ‘Nileteeni Taarifa tukio baya sana’ first appeared on Millard Ayo.