Kutana na Kijana @GodfreyMteule6 (19) mkazi wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu Kigoma mwenye tatizo la kutoona(Kipofu) akiwa na kipaji cha uimbaji ambaye anasema pamoja na kua ni mtu asiyeona lakini hajachoka kupambania ndoto zake na kuamua kuja kwa watanzania kuomba msaada wa kukuza kipaji alichonacho.
Ripota wa Ayo TV Kigoma alifunga safari zaidi kilometers 150 hadi katika kambi ya walimbizi Nyarugusu kufata kipaji hiki ambapo kijana huyu anasema kwao wamezaliwa watoto tisa na yeye ndio mtoto wa kwanza ambaye anasema hawezi kumkufuru Mungu kwa jinsi alivyo.
“Wazazi wangu ni wakimbizi kutoka Congo DRC na mimi nilizaliwa hapa kambini nikiwa naona ila nilipofikisha miezi tisa nilianza kuumwa na kupoteza uwezo wa kuona kabisa,ila kwa sasa napambana na muziki na sijataka kua ombaomba sababu najiona naweza kujitafuta kupitia kipaji hiki kama kweli watanzania wanaona ninafaa kusaidiwa”
Tazama zaidi….
The post Kijana asiyeona mwenye kipaji kikali cha kuimba, anatoka kambi ya Nyarugusu, afunguka mengi kumuhusu first appeared on Millard Ayo.