Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) limeeleza kusikitishwa na hatua ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kumfungia Samuel Eto’o, rais wa FECAFOOT, kushiriki katika mechi za timu ya taifa hilo kwa kipindi cha miezi sita.
Jumatatu wiki hii, FIFA ilisema imemzuia mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Barcelona baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kanuni za usawa katika mchezo na kuwatendea vibaya wachezaji na maofisa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake chini ya miaka 20, mzunguko wa 16 uliohusisha mechi kati ya Brazil na Cameroon, iliyochezwa mapema mwezi Septemb
Ambapo kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba Eto’o, alikabiliwa na mashtaka mawili kutokana na tukio la utovu wa nidhamu aliouonesha kwenye Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 20 nchini Colombia Septemba 11. 2024
Kamati ya nidhamu ya FIFA, imesema kuwa nyota huyo zamani wa Barcelona wa alikiuka vifungu vya 13 (“tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za uchezaji wa haki”) na 14 (“Utovu wa nidhamu wa wachezaji na viongozi”) ya kanuni za nidhamu za FIFA.
The post Shirikisho la Soka la Cameroon lasikitishwa na hatua ya FIFA kumfungia Eto first appeared on Millard Ayo.