Wanajeshi nane wa Israel wameuawa, wakiwemo maafisa watatu wakuu, huku wengine saba wakijeruhiwa vibaya wakati wa mapigano na Hezbollah kusini mwa Lebanon.
Hezbollah ilisema wapiganaji wake walikabiliana na jeshi la Israel lililojaribu kuingia katika mji wa Odaisseh, na kuwalazimisha kurudi nyuma.
Katika taarifa tofauti, kundi hilo lilisema pia lililenga mikusanyiko ya jeshi la Israel, maeneo na miji katika Galilaya ya Juu, Galilaya Magharibi na eneo la Haifa.
Haya yanajiri huku jeshi la Israel likiendelea kushambulia kwa makombora na kuvamia maeneo ya kusini mwa Lebanon, Bekaa na vitongoji vya kusini mwa Beirut kama sehemu ya uchokozi mkubwa unaoendelea dhidi ya Lebanon ambao umeingia wiki yake ya pili.
Israel pia imetangaza miji iliyo karibu na mpaka wake na mpaka wa Lebanon “maeneo ya kijeshi yaliyofungwa”.
Jeshi la Israel limewaagiza wakaazi wa kitongoji cha kusini cha Beirut, haswa Haret Hreik, kuhama mara moja nyumba zao kwa kisingizio cha kuwa karibu na vituo vya Hezbollah.
The post Wanajeshi 8 wa Israel wauawa na wengine kujeruhiwa kusini mwa Lebanon first appeared on Millard Ayo.