Mchungaji wa kanisa la Enendeni church for All Nations kutoka jijini Dar es Saalam ,Mchungaji Christian Saley akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
…….
Happy Lazaro, Arusha .
Wadau mbalimbali mkoani Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha la uzinduzi wa kitabu cha Ubatizo na aina zake utakaofanyika katika kanisa la Elim Pentekoste Unga Ltd oktoba 6 mwaka huu.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mchungaji wa kanisa la Enendeni church for All Nations kutoka jijini Dar es Saalam ,Mchungaji Christian Saley wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo.
Mchungaji Saley amesema kuwa, lengo la uzinduzi wa kitabu hicho ni.ili kuelimisha watu kuhusu maana halisi ya Ubatizo kwani eneo hilo limekuwa likisumbua watu wengi sana .
“Kitabu hiki kitazinduliwa na Askofu mkuu wa Elim Pentekoste jimbo la Arusha ,Askofu Philipo Fisoo ambapo wageni rasmi watakuwa wawili ambao ni Hellena na Clara ambao kwa pamoja watashirikiana katika uzinduzi huo.”amesema.
Amesema kuwa kitabu hicho kitawawezesha watu kujua maana ya Ubatizo halisi wa kibiblia ambao Mungu anautambua .
Mchungaji Saley amesema kuwa,tamasha hill litahudhuriwa na waimbaji mbalimbali ,hivyo kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kumuunga mkono katika tamasha hilo ambalo litakuwa la aina yake .