Gavana wa zamani wa chama cha Republican cha California, Arnold Schwarzenegger, 77, ametangaza kumuunga mkono Mgombea wa Urais wa Chama cha Democratic, Kamala Harris katika uchaguzi wa wiki ijayo.
Schwarzenegger ameandika waraka mrefu kupitia mtandao wa X zamani Twitter akisema kuwa anachukia siasa na amejifunza mengi wakati akihudumu katika majukwaa ya kisiasa kama Gavana wa Chama cha Republican.
Kiongozi huyo wa zamani ambaye alichukua nafasi ya Donald Trump kama mwenyeji wa shindano la The New Celebrity Apprentice mwaka 2016 kwa muda mrefu amekuwa mkosoaji wa wazi wa Trump akimtaja kuwa ni Kiongozi aliyeshindwa.
Schwarzenegger amesema iwapo Trump atashinda “itakuwa miaka minne zaidi ya upuuzi na matokeo ambayo yatatufanya tuwe na hasira, tugawanyike zaidi na chuki zaidi, tunahitaji kufunga mlango wa sura hii ya historia ya Marekani na ninajua kuwa Rais wa zamani Trump hatafanya hivyo.
Ameongeza kuwa “nataka tusonge mbele kama Nchi na ingawa sina maelewano mengi na jukwaa lao lakini nadhani njia pekee ya kufanya hivyo ni pamoja na Harris na Walz.”
The post Arnold Schwarzenegger amuunga mkono Kamala first appeared on Millard Ayo.