Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wameendesha mafunzo kwa viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Mara, Kigoma, Shianyanga,Mbeya, Morogoro, Dar es salaam, Lindi, Mtwara na Pwani juu ya ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi.
Viongozi hao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa, wamejifunza umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi hasa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024, na kupoitishwa kwenye ratiba ya matukiko ya uchaguzi ilki waweze kushiriki kila hatua ikiwa ni pamoja na kuwasisistiza wanawake kujitokeza na kushiriki kikamilifu.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi wakati wa warsha ya mafunzo kwa washiriki kutoka vituo vya Taarifa na Maarifa yakiwa na lengo la kuongeza uelewa kwa washiriki ili ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi kuongezeka, kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na fursa zilizopo katika kuwezesha wanawake kushiriki nafasi za maamuzi yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka vituo vya Taarifa na Maarifa wakichangia mada kwenye mafunzo ya kuwaongezaa ujuzi kuhusu ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi kuongezeka pamoja na kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na fursa hasa kwa uchanguzi wa mwaka 2024 kwenye mafunzo hayo yanayofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mtandano wa Jinsia Tananzaia (TGNP) pamoja na washiriki kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa TGNP kwenye mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.