Mhadhiri Mwandamizi Kitengo cha Afya Kazini na Mazingira Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Vera Ngowi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tafiti mbalimbali za matumizi ya viwatilifu zilizofanyika nchini kote.
Mkuu wa Afya kazini kutoka Wizara ya Afya, Joseph Birago na Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Apolinary Kamuhabwa wakitoa zawadi kwa washiriki wa tafiti mbambali zilizofanyika nchini kote juu ya madhara ya viuatilifu kwa binadamu.
Mkuu wa Afya kazini kutoka Wizara ya Afya, Joseph Birago, akizungumza wakati wa kongamano la kujadili madhara ya viuatilifu kwa binadamu, katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, 2024.
Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Apolinary Kamuhabwa akizungumza wakati wa kongamano la kujadili madhara ya viuatilifu kwa binadamu, lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, 2024.
Na Avila Kakingo
WAKATI matumizi ya Kemikali ya Viuatilifu yakitajwa kuongezeka kwenye uzalisahaji wa mazao ya kilimo pamoja na Shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi, Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema iko haja kwa timu ya wataalamu kufanya tafiti ya matumizi ya Kemikali hiyo ili kunusuru Afya za watumiaji.
Hayo yamesemwa na hadhiri Mwandamizi Kitengo cha Afya Kazini na Mazingira Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Vera Ngowi wakati wa kongamano la kujadili madhara ya viuatilifu kwa binadamu. Katika kongamano lilililofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 06, 2024.
Amesema Shughuli za kilimo, ufugaji, pamoja na utunzaji wa Mazingira ni miongoni mwa vitu vinavyo tajwa kutumia kwa kisia kikubwa viutalilifu ili kulinda Shughuli hizo dhidi ya magonjwa nyemelezi.
Wakati matumizi hayo yakizidi kuongezeka ulimwenguni jambo linalo umiza vichwa vya wataalamu wengi ni uwepo wa athari za matumizi ya Viuatilifu kwa Afya ya binadamu na Mazingira.
Ameeleza kuwa Kuendelea kuwepo kwa hali hiyo kunatoa muanya kwa MUHAS kufanya tafiti inayo jikita kuangalia athari za matumizi ya Viuatilifu na hatimaye kutafuta njia mbadala itakayo tumiwa pasipo kutoa madhara ya kiafya.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Apolinary Kamuhabwa amesema kumekuwa na changamoto za matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu kwenye mazao au wanyama licha ya wataalamu kuelekeza baada ya kutumia viuatilifu, kuwe na muda wa kusubiri dawa hizo zitoke kabla ya kutumiwa na binadamu.
“Kuna tatizo la uelewa au presha ya kutaka kuuza mazao haraka, kipindi cha kusubiri masalia ya viuatilifu yatoke hayazingatiwi, ni lazima kutoa elimu kwa wananchi,” amesisitiza
Profesa Kamuhabwa amesema matumizi mabaya ya viuatilifu ikiwemo viwango na aina ya viuatilifu hivyo, huweza kusababisha madhara ikiwemo magonjwa ya ngozi.
Ameongeza kuwa baada ya utafiti, lengo la ni kutoa mwongozo ili kudhibiti matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu.
Mkuu wa Afya kazini kutoka Wizara ya Afya, Joseph Birago amesema viuatilifu vimekuwa vikitumika kuzalisha mbogamboga ikiwemo nyanya na vitunguu lakini maelekezo yanapaswa yazingatiwe na jamii kwa matumizi bora ya viuatilifu.
Ameeleza kuwa viuatilifu vimekuwa vikitumika kwenye kilimo na mifugo na kwamba yanapaswa kuzingatia afya ya jamii, mazingira, viumbe na mimea, pia
kuangamiza viluilui kwenye mazingira hivyo yakitumika vibaya, huathiri afya binadamu na viumbe hai.
Picha za Matukio mbalimbali.
Mkuu wa Afya kazini kutoka Wizara ya Afya, Joseph Birago na Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Apolinary Kamuhabwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watafiti wa Viuatilifu.