Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamlaka zimeshindwa kuendelea na kampeni ya chanjo dhidi ya maambukizo ya Mpox kutokana na uhaba za dozi wakati huu matukio yakiendelea kuripotiwa haswa miongoni mwa watoto.
Kiongozi wa operesheni hiyo Cris Kacita, amesema dozi zilizosalia ni takriban elfu 53 na zitatumika katika magereza ambapo watu wako hatarini zaidi, wakati ambapo wanahitaji zaidi ya dozi 162, 000 kuanzisha mpango huu jijini Kinshasa.
Zoezi hili likiendelea katika mikoa mingine sita, baadhi ya mataifa yaliyoahidi kutoa msaada hayajafanya hivyo.
Kacita ameendelea kusema kuchelewa kuwasili kwa dozi hizo kumechangiwa na utaratibu wa kiutawala, ambao ni pamoja na kutuma ombi rasmi, kutengeneza, kuandaa hati na kupata vibali vya kuagiza, akiongeza kuwa hali hii itafanya kuwa vigumu kutoa chanjo katika maeneo mengine 14 yaliyoathirika.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka wizara ya afya, Kongo imeripoti matukio mapya 45 yaliyothibitishwa na maafa ya watu 16, katika kipindi cha kati ya Oktoba 28 hadi Novemba 2.
The post Kongo yasitisha chanjo ya Mpox baada ya upungufu wa dozi first appeared on Millard Ayo.