Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus
Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora kwa kutoa Huduma
Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania kwa Mkurugenzi wa Sheria na
Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati
Giattas, wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la
Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa
vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus
Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora inayopendwa Zaidi
na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser wakati wa hafla ya kila mwaka ya
utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser ( wa pili kushoto)
akionesha tuzo ya Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi
Kusini mwa Afrika wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za
Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni
wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser na Mkurugenzi wa
Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi.
Irene Sengati Giattas (katikati), wakionesha tuzo za Benki Bora kwa
kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania na Benki Bora
inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika, mara baada ya
kukabidhiwa, wakati wa hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Chaguo la Walaji,
jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa
benki hiyo.