Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amefungua mafunzo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu Usimamizi wa Fedha za Umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) na kuipongeza Kamati hiyo kwa kutekeleza kikamilifu jukumu lake la msingi la usimamizi (oversight) wa fedha za umma na kukuza utawala bora katika nchi hatua ambayo imeendelea kuisadia Serikali kuboresha maandalizi ya hesabu za Serikali, kuimarisha mifumo ya kielekroniki ya usimamizi wa fedha za umma, na kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa bajeti inayoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila Mwaka.








Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (mwenye tai ya Bendera ya Tanzania), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), baada ya kufungua mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati hiyo, yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).