Mwezeshaji kutoka idara ya sayansi ya siasa  na utawala kutoka chuo kikuu cha DSM ,Prof.Bernadeta Killian wakati akizungumza katika mafunzo  hayo mkoani Arusha 
 
Washiriki mbalimbali katika mafunzo hayo walifuatilia mada  mbalimbali zinazoendelea .
…….
Happy Lazaro,Arusha .
Zaidi ya wanawake mia sita kutoka mikoa saba wanatarajiwa kujengewa uwezo kuhusu maswala ya uongozi na ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi .
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na  Mwezeshaji kutoka idara ya sayansi ya siasa  na utawala kutoka chuo kikuu cha DSM ,Prof.Bernadeta Killian wakati akizungumza katika mafunzo  ya uongozi wa  mabadiliko kwa ajili ya wanawake viongozi kwenye ngazi  ya serikali za mitaa yaliyofanyika mkoani Arusha .
Amesema kuwa,wanatoa mafunzo kwa  viongozi wakiwemo madiwani waliochaguliwa, madiwani wa viti maalum,wenyeviti wa serikali za mitaa na wenyeviti wa serikali ya kijiji ,pamoja na wenyeviti wa majukwaa mbalimbali mkoani Arusha .
 Ameongeza kuwa ,kwa hapa Arusha wanatoa mafunzo kwa wanawake 90 kwa ujumla ambapo wakitoka hapo wataenda wilayani Karatu ambapo  lengo la  kutoa mafunzo hayo  ni kujenga uwezo wa wanawake  kama viongozi  na kuwa viongozi  katika kuleta mabadiliko chanya katika  jamii.
Amesema kuwa, wanatoa mafunzo hayo kwenye mikoa  saba ambapo hadi sasa hivi wameshatoa mafunzo hayo katika mkoa wa Dar es Salaam,Tanga, Pwani,Singida,Mtwara, Lindi,  na Arusha ambapo wakitoka hapo hapo wanaenda mkoa wa Kigoma .
Amefafanua zaidi kuwa ,mradi huo.kwa ujumla unafadhuliwa na shirika la  Un Women Tanzania ikishirikiana na serikali ya Finland ambapo unaendeshwa katika ngazi ya Tamisemi .
Ameongeza kuwa,mafunzo hayo waliyafanya 2017 hadi 2020 mradi ukaisha ndo wakapata huo.ufadhili ambapo utofauti wa sasa ni kuwa Un Women imeingia makubaliano na mashirikiano na serikali katika ngazi ya mkoa na halmashauri ambapo unasimamiwa moja kwa moja na serikali za mkoa  na serikali za mitaa (TAMISEMI).
“Tunafanya kazi  kwa karibu kabisa na maafisa maendeleo ya jamii ambao wapo katika ngazi mbalimbali kwani ndio ambao wanatusaidia kutafuta washiriki wanaostahiki  kuingia kwenye hayo mafunzo .”amesema.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo walianza mwaka jana na hivyo ni muhimu kwani ushiriki wa wanwake katika kufanya maamuzi ni mdogo hivyo mafunzo hayo yanatumika kujengea uwezo wanawake ili tuweze kuongeza idadi yao katika vyombo mbalimbali vya kufanya maamuzi kwa kupitia uchaguzi.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii mkoa Arusha ,Blandina Nkini amesema kuwa, tangu mafunzo hayo yaanze kutolewa wameona mabadiliko  makubwa sana hasa kwa zile kata zenye mradi kwani wakina mama wamekuwa na mwamko mkubwa katika kugombea nafasi mbalimbali.
Naye  Mwenyekiti wa  jukwaa la wanawake kata ya Muriet, Miriam Mbise    maarufu kama “mama Simanjiro”, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakumbusha wajibu wao na kuwa na udhubutu katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.








