Â
Na. Saidina Msangi, WF, Ngorongoro, Arusha.
Wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wametakiwa kutumia huduma rasmi
za fedha kutunza fedha zao badala ya kutunza nyumbani ili ziweze kuingia
katika mzunguko wa fedha na kuongezeka thamani.
Rai hiyo
imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro, Bw. Hussein Urughu, alipokuwa akifungua mafunzo ya elimu ya
fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na
Maafisa kutoka taasisi na watoa huduma za Fedha ilipowasili kwa ajili ya
kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha zilizo
rasmi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Alisema kuwa
njia ya kutunza fedha nyumbani si salama kutokana na kuweza kupata
hasara kutokana na majanga ya moto au kuibiwa na hivyo kushauri wananchi
kutumia huduma za benki kutunza fedha ili ziingie katika mzunguko watu
wapate mikopo ili kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
‘’Watu
wanauza mifugo wanakaa na fedha nyumbani ambapo wangeweza kuweka sehemu
nyingine ikazaa faida, wengine wanaingia vikundi vya kukopeshana bila
kufuata taratibu na baadaye wanadhulumiwa, hivyo ni matarajio yetu kuwa
elimu ya fedha mtakayoitoa itawafungua wananchi kuondokana na changamoto
hizo,’’alisema Bw. Urughu.
Alisema kuwa masuala ya fedha
yanafanyika kimazoea katika jamii kwani sheria kanuni na taratibu za
fedha hazifuatwi hivyo elimu ya fedha ni chachu kwa wananchi wa
Ngorongoro kupata uelewa wa namna bora ya kutunza na kutumia fedha zao
kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Aidha, alisema kuwa
elimu ya fedha itawasaidia wananchi kuweza kujua namna ya kuweka akiba,
umuhimu wa bima, jinsi ya kuwekeza pamoja na kujipanga vema kutumia
fursa za mikopo inayotolea na Halmashauri ili kuweza kujikwamua
kiuchumi.
Naye Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya
Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya,
alieleza kuwa ni muhimu kila mwananchi kuhakikisha kuwa wanachukua mkopo
katika taasisi za fedha zilizosajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania.
‘’Unapoenda
kukopa hakikisha kuwa taasisi imesajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania
lakini pia ni muhimu kuangalia riba ili kujiepusha na riba zisizofuata
sheria kanuni na taratibu ambazo ndio zinasababisha kuwa na mikopo
inayojulikana kama kausha damu kwani riba ni kandamizi,’’, alisisitiza
Bw. Kibakaya.
Aidha, Bw. Kibakaya aliwaeleza wananchi hao kuwa
bila kujali aina ya shughuli wanazofanya uwekaji wa akiba ni muhimu kwa
maisha ya sasa na baadaye hivyo ni vema kuwa na mipango ya mapato na
matumizi huku wakitoa kipaumbele katika upande wa kuweka akiba.
Naye
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi
za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga,
alisisitiza kuwa dhamana zinazowekwa kwa ajili ya mikopo ni lazima
zifanyiwe tathmini ili kujua thamani halisi ya mali inayowekwa dhamana.
‘’Unapotaka
kuweka dhamana kwenye mali ambazo hazihamishiki usiweke hati ya kiwanja
au nyumba bila kutathmini kujua thamani halisi kwani endapo utashindwa
kurejesha mkopo maafisa wasio waaminifu wanaweza kusababisha mali hiyo
kuuzwa kwa bei rahisi ukafilisika na mkopo unakuwa haujaisha,’’
alisisitiza Bw. Myonga.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha
iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na watoa huduma za Fedha
inaendelea na programu ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ngorongoro ambapo makundi ya wakulima, wafungaji, na
wajasiriamali yanatarajiwa kufikishiwa elimu hiyo.Â
Afisa
Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha,
Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, wakati Timu ya
Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau
mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha
utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro mkoani Arusha.
Afisa
Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga na Mchumi kutoka Wizara ya
Fedha, Bw. Renatus Lucas, wakimkabidhi zawadi ya fulana Bw.Roy Mollel, baada ya
kutoa elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha
iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa
ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha
vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Hussein Urughu,
akipokea vipeperushi kuhusu elimu ya fedha kutoka kwa Afisa Sheria Mwandamizi
kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Bw. Ramadhani Myonga, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha
iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa
ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha
vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Baadhi
ya wananchi wa Tarafa ya Loliondo, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa
kuhusu elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha
iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa
ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha
vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Afisa
Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha,
Bw. Stanley Kibakaya (kushoto) na Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya
Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw.
Ramadhani Myonga (kulia), wakiwa na wananchi wakionesha baadhi ya mada
walizojifunza katika mafunzo ya elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka
Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali,
ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma
za fedha vijijini, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani
Arusha.
Afisa
Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga (kulia), na Meneja wa Benki
ya NMB Ngorongoro Bw. Gabriel Thomas Chabai, wakimkabidhi zawadi ya fulana Bw.
Felician Pius Bukene zawadi ya fulana baada ya kujibu maswali kuhusu elimu ya
fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa
kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya
fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Halmashauri
ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
 Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Hussein Urughu
(Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya
Fedha, na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya
kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini katika
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka
Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya,
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Daniel Bura na
Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha wilaya hiyo Bi. Gloria Nampesya. Kushoto ni
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, Afisa Tarafa ya Loliondo
na Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Bw. William Ndosi na Mchumi kutoka Wizara ya
Fedha, Bw. Renatus Lucas.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Ngorongoro, Arusha)
​Â