▪️Ampongeza Rais Samia kwa kwa maono ya kukuza sekta ya Madini
▪️Avutiwa na aonesha utayari wa kusaidia VISION 2030
▪️Apongeza mpango wa serikali wa kuongeza thamani madini mkakati nadani ya nchi
📍Dar es salaam
Naibu
katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Mh. Amina J. Mohamed ameipongeza
serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan
kwa mkakati wa kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia na utafutaji madini
nchini.
Naibu Katibu Mkuu Amina Mohamed ameyasema hayo leo
wakati wa mkutano wa pembeni wa Mkutano wa Nishati alipokutana na Waziri
wa Madini Mh. Anthony Mavunde.
“Naipongeza Tanzania chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia ambao umekuja na ubunifu mkubwa katika maeneo mbalimbali.
Mpango
wa kufanya utafiti wa kina kupitia Vision2030 ni mpango ambao tunauunga
mkono kwa kuwa una lengo la kubaini madini ambayo mnayo na hivyo
kujiapanga vyema juu ya uvunaji wa madini hayo.
Dunia hivi sasa
ina mahitaji makubwa ya madini mkakati,Tanzania imebarikiwa kuwa na
madini hayo kwa uwingi hivyo suala la uongezaji thamani,utunzaji wa
mazingira na kulinda jamii zinazoishi katika maeneo ya uchimbaji wa
madini ni vyema yakazingatiwa wakati wa uandaaji wa mkakati maalum wa
uvunaji wa madini ya kimkakati.
Umoja wa Mataifa kupitia programu
zake mbalimbali za utunzaji wa mazingira ipo tayari kuunga mkono
jitihada hii kubwa ya serikali ya Tanzania“Alisema Mh. Amina Mohamed
Akizungumza
katika mkutano huo,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema
kipaumbele cha sekta ya Madini kwa hivi sasa ni kufanya utafati wa kina
ili kuiwezesha nchi kupata taarifa za kiwango na ubora wa madini
iliyonayo.
Aliongeza kwamba,Utafiti wa kina utaleta matokeo
chanya kwenye maeneo ya kijamii na kiuchumi na hivyo kusaidia kuchochea
maendeleo ya Tanzania,kwakuwa pamoja na mafanikio yote ya kwenye sekta
ya madini eneo ambalo limefanyiwa utafiti ni asilimia 16% ya eneo la
nchi nzima.