Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionensia Mjema, akitoa Elimu ya Fedha kwa Wanafunzi walioshiriki semina ya Elimu ya Fedha kuhusu Umuhimu wa kuweka Akiba iliyofanyika katika Sekondari ya Mwika, Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Wanafunzi wa Sekondari ya Mwika wakisikiliza Elimu ya umuhimu wa kuweka Akiba kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Bi. Dionensia Mjema (hayumo pichani) iliyofanyika katika Sekondari ya Mwika, Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salimu Kimaro, akitoa elimu ya fedha kuhusu Akiba na Bajeti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwika iliyoko Kata ya Mwika Kaskazini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salimu Kimaro, akitoa elimu ya fedha kuhusu Akiba na Bajeti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mangi Mariale iliyoko Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Mkuu kutoka Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi akiwapongeza wanafunzi waliojibu maswali vizuri baada ya kupata Elimu kutoka kwa Wataalamu wa Wizara ya Fedha katika Shule ya Sekondari ya Mareale iliyopo Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
Picha ya Pamoja ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mareale mara baada ya kumaliza semina ya Elimu ya Fedha iliyofanyika katika shule hiyo iliyopo Kata ya Mwika Kusini Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro.
…………….