Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Mashariki Mohamed Omary akizungumza jambo katika hafla iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni kwa ajili ya kuukaribisha mwaka 2025, kuwaaga wastaafu, kuwatambua baadhi ya wateja wakubwa kwa kuwapa zawadi iliyofanyika Februari 15, 2025, Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola akimlisha keki mteja katika hafla ya kuukaribisha mwaka 2025, kuwaaga wastaafu, kuwatambua baadhi ya wateja wakubwa kwa kuwapa zawadi iliyofanyika Februari 15, 2025, Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Mashariki Mohamed Omary (wa nne kutoka kushoto) akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi wastaafu wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao kwa Shirika.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Mashariki Mohamed Omary (wa nne kutoka kushoto) akikabidhi zawadi kwa wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao kwa shirika.
Afisa Habari, Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Lucia Renatus (wa kwanza kushoto), Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Steven Maganga pamoja na wafanyakazi wengine wakiwa katika hafla ya kuukaribisha mwaka 2025, kuwaaga wastaafu pamoja na kuwatambua baadhi ya wateja wakubwa kwa kuwapa zawadi.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni wakifurai.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni wakifanya mazoezi ya kukimbia (Jogging) kwa ajili ya kuimarisha afya ikiwa ni sehemu ya hafla ya kuukaribisha mwaka 2025
………
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke na Kigamboni wamefunga mwaka kwa kishindo kwa kufanya tafrija ya kipekee ya kuukaribisha mwaka 2025 pamoja na kuwaaga wastaafu kwa kutoa mchango mkubwa kwa Shirika hilo.
Hafla hiyo imefanyika Februari 15, 2025 jijini Dar es Salaam ikiwa ni fursa ya uongozi kutoa shukrani na kuthamini juhudi za wafanyakazi na pamoja na kuwatambua baadhi ya wateja wakubwa kwa kuwapa zawadi.
Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi TANESCO Kanda ya Mashariki Mohamed Omary, amewataka wafanyakazi wa Mkoa wa Temeke na Kigamboni kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya shirika ikiwemo kutoa huduma bora ya umeme kwa wateja.
Omary amewapongeza wastaafu wote kwa kulitumikia Shirika kwa bidii na uaminifu mkubwa katika kipindi chote cha kazi yao. “Tunawatakia kila la heri katika maisha yenu mapya na tunaomba mkawe mabalozi wazuri huko muendapo”.
Amempongeza Meneja wa Mkoa wa Temeke na Kigamboni kwa kuwaongoza vizuri wafanyakazi pamoja na kudumisha umoja na mshikamano.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola, amewasihi wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mwaka 2025 ili kuhakikisha shirika linatoa huduma bora ya umeme kwa wateja.
Wakizungumza katika hafla hiyo, Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni, wameushukuru uongozi kwa kufanikisha hafla hiyo, kwani imewafanya kujumuika pamoja na kuongeza upendo na ushirikiano baina yao, huku wastaafu wakitoa shukrani na kuonesha furaha ya kuagwa na kuingia kwenye maisha mapya ya ustaafu.
Katika kufanikisha hafla hiyo asubuhi Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni wameshiriki michezo mbalimbali pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia (Jogging) kwa ajili ya kuimarisha afya.