CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimefanya mabadiliko katika mchakato wa upatikanaji wa wagombea kuelekea uchaguzi mkuu, hakuna kupita bila kupingwa kwani zitapigwa kura za ndio na hapana kwa wagombea katika mchakato huo.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla alieleza hayo leo Machi 7,2025 wakati akizungumza katika mkutano wa ndani uliofanyika kuzungumza na viongozi wa chama ngazi ya tawi, kata na Wilaya katika Wilaya ya Temeke Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano mkoani humo.
Makalla amesema CCM imefanya marekebisho makubwa mawili ikiwemo uchujaji wa wagombea kabla ya kura za maoni tofauti ya ilivyokuwa hapo hapo awali lilikuwa likirudi jina moja na kuchapita bila kupingwa lakini mwaka huu itakuwa tofauti ili wabunge na madiwani wapate usalama na utulivu.
“Badiliko lingine kubwa yale mambo ya kupita bila kupingwa sasa hivi hayapo tena, yaani wewe ndani ya chama chako ukapit abila kupingwa na ukataka na nje upite bila kupingwa halipo hilo ni sehemu ga mabadiliko sasa hivi utapigiwa kura za ndio na hapana,” amesema Makalla.
Ameongeza kuwa hapo awali watu walikuwa wanachukua fomu na kurudishwa jina moja lakini mara hii itakuwa tofauti kwani utafanyika mchujo wa awali kwa kurudishwa majina matatu ambayo yatapigiwa kura za ndio na hapana, hivyo hakuna atakayepita bila kupingwa.
#CCMImara
#VitendoVinasauti
#KaziIendelee