RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkaribisha tende Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi kwa ajili ya kufungulia saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar,iliyofanyika jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Wananchi wa Makundi Maalumu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,katika Iftaar aliyowaandalia katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, iliyofanyika jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
MTOTO Samir Idrisa akipata futari maalumu iliyoandiliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wa Makundi Maalumu iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja iliyofanyika jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar iliyoandaliwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja iliyofanyika jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar aliyowaandaliwa Wananchi wa Mkoa huo,iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Wananchi katika kuitikia Dua ikisomwa na Mifti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, iliyofanyika jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalumu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa, baada ya kumalizika kwa hafla ya Iftaar iliyoandaliwa kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana 12-3-2025.(Picha na Ikulu)