VICTOR MASANGU, KIBAHA
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pangani ilyopo katika Halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutenga kiasi cha shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji ambao utakwenda kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi hao na maeneo mengine ya jirani.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Dawasa Wilaya ya Kibaha Halfa Ambokile wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Panagni ambao umendaliwa na Jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mji kwa lengo la kuweza kuzungumza na wananchi ikiwa pamoja na kusikiliza kero na chanagmoto zinazowakabili kwa ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo suala la huduma ya maji katika eneo hilo.
Meneja huyo amesema kwamba kwa sasa wameshaanza maandalizi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.9 amabzo zimetolewa na serikali na kwamba wanatarajia kuanza rasmi zoezi zima la utekelezaji ifikapo Aprili 15 mwaka huu na kwamba mradi huo utaweza kusambaza maji katika mitaa ipatayo sita pamoja na maeneo mengine ya jirani.
“Kwa sasa tumeshaanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa ambapo tunatarajiwa kujenga tanki kubwa lenye ujazo wa milioni 6 amabapo mradi huo utekelezaji wake utatumia muda wa miezi nane hadi 12 kumalizika na baada ya hapo wananchi wataanza rasmi kupata huduma ya maji safi na salama katika mitaa saba ya kata ya Pangani ambayo iliyokuwa badio haina huduma ya maji,”amesema Meneja huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amesema kwamba juhudi kubwa zimefanywa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassa kwa kuweza kutenga fedha mbali mbali ambazo zimekwenda kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata ya pangani ikiwemo, afya, elimu, miundombinu na barabara pamoja na mradi mkubwa wa maji ambao utaweza kutatua kero na changamoto za wananchi hao.
Aidha Mgonja amemshukuru kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe: Silvestry Koka kwa kuweza kuwapambania wananchi wa kata hiyo katika suala la kuwaletea maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwa sambamba na kuweza kusikiliza changamoto mbali mbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Pangani Jitihada Hussen amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga kiasi cha shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji ambao utakwenda kuondoa kabisa changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili wananchi kwa kipindi kirefu.
“Kwa kweli mimi kama mwenyekiti nampongeza kwa dhati Rais wetu kwa juhudi zake za kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo suala zima la kutuangalia wananchi wa Pangani kwa jicho la tatu kwa kutenga fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya kutekeleza miradi mkiubwa ya maji ikiwa sambamba na Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kusikiliza kero za wananchi,”alisema Mwenyekiti huyo.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Pangani hawakusita kumpongeza kwa dhati Mbunge wao wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuweza kuwa mstari mbele katika katika kuhakikisha anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kulivalia njuga suala la kuwepo kwa mradi mkubwa wa maji ambao utaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya Pangani na maeneo ya jirani.
Kukamilika kwa mradi wa Pangani uliopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoa wa Pwani unatarajiwa kuanza utekeezaji wake rasmi kuanzia Aprili 15 mwaka huu ambao utaweza kuondoa kero na chanagmoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanakosa huduma hiyo kwa kipindi kirefu.


