*Arusha
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Madini, Machi 22, 2025, walitembelea Kituo cha Jemolojia Tanzania ( TGC) kilichopo jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya Wajumbe hao kujifunza kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Kituo hicho.
Katika ziara hiyo, pia walitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Jengo la ghrorofa Nane linalotarajiwa katika Kituo hicho pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya shughuli za utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito na miamba yanayotolewa na Kituo hicho.
Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Mratibu Wa Kituo hicho Ally Maganga alisema kwa sasa Kituo hicho kina jumla ya wanafunzi 110 wanaosoma masomo ya muda mrefu na Sita wanachukua mafunzo ya muda mfupi.
“Tumepiga hatua kwenye uzalishaji wa mapambo kutokana na kupata vifaa vya teknolojia ya juu na ni imani yangu baada ya kukamilika kwa mradi huu Kituo hiki kitapiga hatua zaidi,” alisema Maganga.