NJOMBE .
Wananchi wa mtaa wa National Housing uliyopo kata ya Njombe mjini wilayani Njombe wamelitaka jeshi la polisi kupunguza matumizi ya nguvu pindi wanapomhoji mtuhumiwa wa kitendo cha ualifu ikiwa ni pamoja na kutupia shoti umeme ili kushinikiza kukiri kutenda kosa na badala yake lihoji kwa mujibu wa kanuni na taratibu za jeshi la kusaka ukweli hadi pale utakapopatikana.
Akizunungumza katika mkutano wa hadhara uliyoitishwa na tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini(THBUB) wenye nia ya kutoa elimu ili kuwajengea uwezo wananchi wa kufahamu haki za binadamu na utawala bora ambapo bwana Paskal Mng’ong’o amesema kuna shida kubwa na uvunjwaji wa haki za watu polisi kwasababu wanatumia nguvu kubwa kulazimisha watuhumiwa kukiri kutenda kosa kwa kuwapa adhabu kali hivyo wanaomba THBUB kuona nanba ya kuwasaidia .
Akitoa ufafanunuzi kuhusu nguvu na mpaka wa tume hiyo kamishana wa tume hiyo Dr tomas Masanja amesema endapo ni kweli kuna rai aliyepigwa shoti ya umeme ni kosa kisheria hivyo endapo likijitokez a tena muathirika apige simu ili maofisa uchuguzi wa tume waweze kufanya uchunguzi na kisha kumfungulia kesi askari mmoja aliyejusika na sio jeshi la polisi kwa ujumla wake
Awali Said Zuberi ambae ni afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
ametoa elimu kuhusu sheria ya mtoto na kisha kuikumbusha jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kunapotokea mikasa ya ubakaji na ulawiti ili watendaji waweze kuchukuliwa hatua.
Katika hatua nyingine amefundisha sheria ya faragha mazuri yake na athari zake kwa atakae kutwa na kosa hilo

