Na Prisca Libaga, Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Colombo Plan Drug Advisory Programme (CP-DAP) tarehe 28.03.2025 imehitimisha rasmi mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wawakililshi kutoka Asasi 25 za Kiraia zinalizopo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambazo zinapambana na dawa za kulevya yaliyofanyika katika Ukimbi wa Amani Center uliopo Kaloleni jijini Arusha.
Mafunzo hayo ya siku tano yalihusu Mtaala wa Kimataifa wa Utoaji Elimu Kinga Sahihi Dhidi ya Tatizo la Dawa za Kulevya (Universal Prevention Curriculum-UPC).
Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku tano mfululizo kuanzia tarehe 24.03.2025 ambapo Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude.
Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Machi 24, 2025 alikuwa Joseph Modest Mkude Mkuu wa Wilaya Arusha na Machi 28, 2025 yalifungwa rasmi na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini Ndg. Gerald Mwaitebele ambapo pamoja na mambo mengine aliyoeleza wakati wa hotuba yake alipongeza jitahada kubwa zinazofanywa na Mamlaka katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuhimiza kwa kuziomba Asasi za Kiraia ziendelee kutoa elimu iliyosahihi kwa umma inayotegemea tafiti zilizothibishwa kisayansi.
Mwisho, Washiriki wote wa mafunzo hayo walipatiwa vyeti kutoka Taasisi ya Colombo Plan Drug Advisory Programme (CP-DAP) kwa kushirikiana na DCEA ambavyo vinatambulika kimataifa.
Ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini itaendelea kuwajengea uwezo wadau wake mbalimbali wanaofanya kazi ya udhibiti wa dawa za kulevya ili kuhakikisha kunakuwepo na Wataalamu wakutosha waliobobea katika utoaji elimu kinga sahihi juu ya madhara yatokanayo na tatizo la dawa za kulevya.




