Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Zainab Telack ameongoza Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Maonesho kilichofanyika Ruangwa huku akitaja Juni 11 hadi 14, 2025 kuwa tarehe ya msimu wa pili wa monesho ya madini katika mkoa huo ambayo yataambatana na mnada wa madini
Baadhi ya a washiriki wa kikao cha maandalizi ya wiki ya madini Lindi.
Na Fredy Mgunda, Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Zainab Telack ameongoza Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Maonesho kilichofanyika Ruangwa huku akitaja Juni 11 hadi 14, 2025 kuwa tarehe ya msimu wa pili wa monesho ya madini katika mkoa huo ambayo yataambatana na mnada wa madini,Maonesho hayo yatafanyika katika viwanja vya madini Ruangwa Mkoani Lindi.
Telack akiongoza kikao hicho kilichowakutanisha Viongozi wa Serikali Mkoa wa Lindi, wawakilishi wa makampuni ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini, wachimbaji wadogo wadogo, Taasisi mbalimbali za Serikali na kifedha, Bodi ya korosho na vyama vya ushirika, vikiwemo Lindi Mwambao na RUNALI, amesema maonesho ya mwaka huu yatakuwa yatofauti sana hivyo kila mmoja kwanafasi yake anaalikwa kushiriki.
Maonesho ya Madini Mkoa wa Lindi yanatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa wadau wa sekta hiyo kutangaza fursa za madini, kuimarisha usimamizi wa rasilimali madini, na kuhamasisha uwekezaji endelevu kwa maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla.
Telack ameweka mkazo katika msimu mpya wa pili wa madini wa mwaka huu kufanyika kwa mnada mkubwa wa madini ambao utatoa fursa kwa wachimbaji na wadau wa madini kuona, kuuza na kununua vito mbalinbali vya thamani vinavyotoka Mkoani Lindi.