Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya akili,kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe,,Dkt.Veronica Lyimo,akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 5,2025 katika banda la Hospitali hiyo wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Afya Kitaifa yanayoendelea katika kituo cha Mikutano Cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Na Alex Sonna-DODOMA
MAADHIMISHO ya wiki ya Afya 2025 yanaendelea Jijini Dodoma ambapo wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kituo cha mikutano Cha Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa afya ya akili.
Upimaji huo umeanza Aprili 3 mwaka huu na unatarajiwa kumalizia Aprili 8 mwaka huu ambapo huduma mbalimbali za upimaji na uchunguzi wa awali zinafanyika.
Huduma zinatolewa na wataalamu bingwa na bobezi kutoka Hospitali za Mirembe,Benjamini Mkapa,Bugando,Moi,KCMC,Ocean Roads,Kibong’oto.
Akizungumza leo Aprili 5,2025 katika Banda la Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe,
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya akili,kutoka katika Hospitali hiyo,Dkt.Veronica Lymo amesema katika wiki ya Afya wamejiandaa kutoa huduma kwa watanzania wote.
Amesema wapo katika wiki hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali kwa watu wote na iwapo watagundulika wana changamoto watahakikisha wanapata tiba sahihi.
“Tunawakaribisha wote kwa wingi hapa nia ni kuwasaidia ukipata msaada mapema unazuia shida ambayo ingetokea baadae,”amesema Dk Veronica.
Hata hivyo amesema wagonjwa wengi waliopo katika Hospitali yao ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 18 mpaka 40.
Amesema visababishi huwa kibailojia ama kisaikolojoa huku akidai vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanapitia changamoto nyingi ndio maana wapo kwa wingi katika hospitali hiyo.
Amesema ili kuondokana na changamoto hiyo wanatakiwa kufanya uchunguzi wa awali ambapo watapatiwa tiba.
Amesema wamekuwa wakihamasisha wananchi kwa kutoa elimu ambapo mpaka sasa wamezunguka katika Mikoa mitano ili watu watambue nini maana ya afya ya akili,changamoto ya Afya za akili na magonjwa ya akili.
Amesema Hospitali ya Mirembe inahusika na magonjwa ya akili na changamoto ya afya ya akili huku akidai wanahudumia wagonjwa wote wa magonjwa ya ndani.
Amesema kutokana na Teknolojia kuendelea kutumika wanaangalia namna ya kutumia akili mnemba katika utoaji wa huduma hasa katika magonjwa ya afya ya akili.
Kwa upande wake Dk Abasi Msaji kutoka Hospitali ya amesema wanatoa huduma za upimaji wa sukari,pressure,ushauri kuhusu uzito.
Amesema Hospitali hiyo ni kubwa wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo moyo na magonjwa mbalimbali.
Mkazi wa Dodoma Makulu Emmanuel Masawe amepongeza utoaji wa huduma hizo ambapo amedai wamesikilizwa vizuri.
Amesema wanapenda huduma hiyo iwe endelevu kwa sababu hospitalini ni gharama na foleni ni kubwa,gharama kubwa.
“Tunatamani Sana Kila Mtanzania aweze kufikia Jakaya Kikwete kupata huduma rafiki na nzuri hapa tunapima magonjwa yote,”amesema Bw.Masawe
Amesema amepima mkojo pamoja na pressure ambayo hajawahi kupima katika maisha yake.
Ukifika Jakaya Kikwete utafanya upimaji wa Figo, Magonjwa ya Moyo na Mishipa, Upimaji wa Shinikizo la Damu (BP) Ugonjwa wa Kisukari, Kifua Kikuu,Uzito na hali ya lishe,Huduma za Kinywa na Meno,Upimaji na matibabu ya Macho,Huduma za uzazi wa Mpango,Upimaji wa Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi.
Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi (HPV),Msaada wa saikolojia na Afya ya Akili,Elimu ya Lishe, Upimaji wa Saratani