Na Prisca Libaga Arusha
OFISI YA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA KANDA YA KASKAZINI KWA NIABA YA KAMISHNA JENERALI WA DCEA ARETAS LYIMO LEO TAREHE 09.04.2025 IMETEKETEZA KIASI CHA KILOGRAMU 94.828 CHA DAWA ZA KULEVYA AINA MIRUNGI KATIKA DAMPO LA H/SHAURI LILILOPO ENEO LA MAJI YA CHAI WILAYANI ARUMERU.
UTEKETEZAJI VIELELEZO HIVI UMEHUSISHA WADAU WOTE MUHIMU KWA MUJIBU WA TAKWA LA KISHERIA.
UTEKETEZAJI WA VIELELEZO HIVYO NI MATOKEO YA MAFANIKIO YA OPERESHENI YA UKAMATAJI WA WATUHUMIWA WA BIASHARA NA WASAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI ILIYOFANYIKA TAREHE 04.04.2025 KATIKA MAENEO YA KIJENGE KUSINI KATA YA KIMANDORU MKOANI ARUSHA AMBAPO JUMLA YA WATUHUMIWA SITA WALIKAMATWA KWA MAKOSA YA KUHUSIKA NA UHALIFU HUO.
MAMLAKA INATOA RAI KWA WANANCHI WANAOISHI KATIKA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI AMBAYO NI ARUSHA, KILIMANJARO, MANYARA NA TANGA KUTOJIHUSISHA KWA NAMNA YOTOTE NA DAWA ZA KULEVYA KWANI ADHABU YAKE NI HADI KIFUNGO CHA MAISHA JELA.




