Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amempongeza Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel kwa kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na kutekeleza majukumu yake kwa wakati na kuleta tija kwa Wizara na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia utendaji wa Dkt. Mollel, Waziri wa Afya Mhe. Mhagama, amesema kuwa amekuwa msaidizi mwenye msaada mkubwa katika sekta ya afya, huku akimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan kwa kumteua kuwa msaidizi katika Wizara hiyo pamoja na kumuacha aendelee kufanya kazi akiwa Naibu Waziri.
“Nakuombea kila la kheri, naamini kwa utendaji wako uliotukuka na jinsi unavyojitoa, kwa mwaka huu 2025 mambo yako yatakuwa mazuri” amesema Mhe. Mhagama.