Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Rear Admiral Ameir Ramadhan Hassan amefanya mapokezi ya Meli Vita aina ya INS SAGAR OPV ya Jeshi la India leo tarehe 12 Aprili 2025 katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mapokezi ya Meli hiyo ni moja ya maandalizi ya zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia Kamandi ya Jeshi la Wanamaji na Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India, zoezi linalojulikana kama Africa India Key Maritime Engagement (AIKEYME) ambalo litashirikisha na Majeshi mengine ya nchi rafiki.
Zoezi la Wanamaji linatarajiwa kufanyika eneo la Bandari ya Dar es Salaam na Bahari ya Hindi kuanzia tarehe 13 Aprili, 2025 na kufungwa tarehe 18 Aprili, 2025. Zoezi hilo litawezesha vikundi shiriki kuongeza ujuzi na uelewa wa pamoja wa kukabiliana na changamoto za kiusalama hasa katika maeneo ya baharini.