Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Zuwena Farah akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha .

Baadhi ya waendesha baiskeli hao wakiwa katika kikao.hicho na waandishi wa habari jijini Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Zaidi ya waendesha baiskeli 200 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kushiriki msafara wa Twende Butiama kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika falsafa za maendeleo hasa katika kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,Mwenyekiti wa msafara wa Twende Butiama Gabriel Landa amesema mwaka huu wameamua kubadili njia na kupita kaskazini ili kuona mambo mbalimbali yaliyofanywa na baba wa Taifa ikiwemo azimio la Arusha.
Landa amesema kwa kutumia baiskeli zao, vijana kutoka mikoa mbalimbali wanapita vijiji na miji, wakibeba ujumbe mmoja muhimu wa uzalendo wa kweli bado upo, na unaishi ndani ya kizazi kipya.
“Twende Butiama si tu kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere bali pia mwamko ni sauti ya mshikamano, afya ya jamii, na maendeleo ya vijana kupitia michezo na usafiri”amesema Landa .
Ameongeza kuwa, katika kila mtaa wanaopita, vijana hawa wanakutana na wenzao wanabadilishana mawazo, wanahamasishana,juu ya yote, wanakumbusha umuhimu wa kuenzi historia na misingi ya taifa.
Naye Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Zuwena Farah amesema katika msafara huo watawezesha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti na kuboresha mazingira ya elimu jumuishi na afya.
Zuwena amesema kuwa kwa sasa matembezi hayo yataanzia rasmi Mkoa wa Arusha tofauti na kipindi cha nyuma ambapo matembezi hayo hufanyika katika mikoa mingine.
“Tunao wadau wengine ambao wameshirikiana na sisi na kwamba ipo misaada itakayotolewa ikiwemo baiskeli kwa watoto wenye uhitaji ili kupamba matembezi hayo kuelekea makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere “amesema.
“Kadri safari inavyoendelea, na kila kilomita inapopungua, ujumbe wa Twende Butiama unazidi kugusa mioyo ya Watanzania.”amesema Zuwena.
Twende Butiama itafanyika kwa muda wa siku 10 kwa umbali wa zaidi ya kilomita 1500 kupitia katika mikoa 11..