Na Silivia Amandius
Kagera.
Kampeini msaada wa kishereia ya mama samia imefanikiwa kuyafikia makundi mbalimbali yakiwemo makundi ya maafisa usafirisha maarufu kama bodaboda katika halmashauri ya wilaya ya kyerwa.
Akizungumza na maafisa usafirishaji hao katika mojawapo ya mkutano wa adhara uliofanyika kata Isingiro bi Getruda Mwiga kutoka katika timu ya msaada wakisheria ya mama samia amewasihi kuhakikisha wanatumia kampeini hiyo kupokea elimu bora ili kuweza kutambua ni kwa namna gani wanaweza kufahaumu haki zao katika kuchukua chombo cha moto kwa mtu na ni nini kinatakiwa kufanyika.
Pia ameongezea na kusema kuwa wapo baadhi ya matajiri wanaotoa pikipiki kwa maafisa usafirisha na baadae kuwazunguka pale wanapokaribia kumaliza mikataba yao wanatumia nafasi hiyo kuwazunguka na kuwataka kuwa makini na kutunza vizuri usafiri wao.
“Niwaombe kitu kimoja tuhakikishe tunaandikiana na tajiri wako anaekupa pikipiki ili kuepuka kukuzunguka ua kukugeuka na kusema ulimwibia pikipiki kwahiyo tujue na kuelewa kuandikiana na matajiri wetu ni moja wapo ya kuepuka migogoro hapo baadae maana yapo matukio mengi ya wizi wa pikipiki ukiijua sheria unakuwa umejilinda pia”
Nao baadhi ya maafisa usafirishaji akiwemo ndg. Linus George na Joa Josephat wameieshukururu timu ya msaada wa kisheria ya mama samia na kumshukuru rais Samia kwani amewafikia hata wananchi wa chini kabisa kwa kuwapa elimu kuhusu sheria mbalimbali na kutambua haki na wajibu wao katika kazi yao ya usafirishaji.
Wameongeza na kusema kuwa kupitia elimu waliyoipata itaenda kuwa chachu ya kupunguza hata vitendo vya ukatili wa kijinsia na uharifu katika jamii kwani maafisa usafirishaji wamekuwa wakihusishwa zaidi katika matendo hayo .