Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo.
Siku hii njema ikawe pia ya tafakari kwetu sote juu ya upendo wetu kwa Muumba wetu na wenzetu; juu ya kujitoa kwa bidii na weledi katika utekelezaji wa majukumu yetu popote pale tulipo; juu ya kuendelea kujenga jamii inayoishi katika kweli; na juu ya haki ambazo daima huambatana na wajibu kwetu sote.
Kwa pamoja, tuendelee kuliombea Taifa letu kheri, huku tukiishi na kutenda yale yanayoiwezesha nchi yetu kuendelea kubaki kuwa moja, imara, yenye amani na utulivu.