Na Oscar Assenga, TANGA
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM) wamefanikiwa kusajili zaidi ya wanachama 550,000 kwa mkoa wa huo kwa mfumo wa kieletroniki kwa muda wa siku 10 wakiziita siku 10 za moto, katika zoezi hilo wamefanikiwa kuhakiki Taarifa za wanachama wao na sasa wako kwenye siku 10 za moto za kugawa kadi za kieletroniki kwa Wilaya za Mkoa huo baada ya usajili na uhakiki kukamilika.
Akizungumza na Mtandao huu,Katibu wa Siasa,Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Tanga Ndugu Samwel Kiondo Mngazija alisema kwamba wanaendelea na zoezi hilo katika Wilaya mbalimbali za mkoa huo huku usajili nao ukiwa unaendelea na kwa sasa kwenye mfumo wana wanachama zaidi ya 700,000 mpaka 800,000 ambao wamesajiliwa.
“Zoezi hili la uhakiki wa wanachama wetu tunalifanya kwa umakini mkubwa na weledi na tunazunguka Mkoa mzima kwa siku 10 za moto kugawa kadi za kieletroniki za CCM kwa wanachama wetu na tunaendelea na uhakiki wa Taarifa na usahihishaji wa taarifa za wanachama wetu na zoezi la usajili wanachama wapya linaendelea”Alisema
Aidha alisema kwamba awali kwenye mkoa wa Tanga walikuwa na zaidi ya wanachama 200,000 wanatarajia kufikiwa na mfumo wa kadi za kieletroniki ambao usajili ulianza 2018 na mwaka huu walihuisha zoezi kwa maana watu wengi walikuwa hawajaingia kwenye mfumo na usajili ulikuwa unaendelea.
“Kutokea mwaka huu tulikuwa na siku 10 za moto ambapo wilaya zote za Mkoa wa Tanga tumezifikia kwa Maelekezo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kuleta Vitendea Kazi kila kata kwa ajili ya kurahisisha usajili na kwenda na kasi kutokana na uhitaji wa kadi kwa wanachama wetu hivyo kupelekea zoezi la siku 10 za moto kuwa na tija kubwa pamoja na Usimamizi wa Jemedari wa Vita Ustadhi Rajab Abrahamani Abdallah Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa” Alisema
Hata hivyo alisema kwamba kila siku wanachama wanajiunga nao kutokana na maendeleo makubwa yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Daktari Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake.