Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Aprili 28,2025 jijini Dar es salaam, amefanya ukaguzi wa magari mapya na ya kisasa kwa ajili ya matumizi ya operesheni mbalimbali za kipolisi.
IGP Wambura amesema Magari hayo pamoja na vifaa vingine vimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa Jeshi hilo.
Akizungumza na Maafisa na askari wa vyeo mbalimbali wakati akifanya ukaguzi huo IGP Wambura amewasisitiza kuendelea kufanyakazi kwa Utii, bidii, weledi na uadilifu huku akitoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Maboresho makubwa aliyofanya kwa Jeshi la Polisi tangu alipoingia madarakani na kulifanya kuwa Jeshi la kisasa na lenye weledi mkubwa katika kutekeleza majukumu yake ya kazi za kila siku.