MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid, akizungumza na wajumbe wa kamati ya wataalamu ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, Wilaya ya Chake Chake walipofika Ofisi kwakwe kuzungumza nae juu ya kampeni hiyo kuanza kutekelezwa.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Mgeni Khatib Yahya, akizungumza na wajumbe wa kamati ya wataalamu ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, Wilaya ya Chake Chake walipofika Ofisi kwakwe kuzungumza nae juu ya kampeni hiyo kuanza kutekelezwa.(PICHA NA MARIYAM SALIM, PEMBA.
MKOA WA KUSINI PEMBA
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Khadid Rashid, amemshukuru Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuja na Kampeni ya Msaada wa Kisheria, kwani kampeni hiyo itaweza kutoa sufrsa kwa wananchi kupata haki zao za kisheria ambazo wamezikosa kwa muda mrefu.
Alisema elimu hiyo itakayotolewa katika shehia mbali mbali ndani ya Mkoa huo, itaweza kutoa faraja kwa wananchi wa maeneo mbali mbali ambao haki zao wamezikosa za kisheria.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyaeleza hayo, wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya wataalamu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, walipofika kujitambulisha na kuanza kazi ya utoaji wa elimu katika shehia mbali mbali ndani ya Mkoa huo.
“kwa Nimpongeze Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa muono wake wa kuja na kampeni hii ya Msaada wa kisheria, kampeni ambayo itaongeza uwelewa na mashikamano kwa wananchi,”alisema.
Alisema katika Mkoa huo zipo changamoto za kisheria, ikiwemo udhalilishaji, wananchi kukosa haki za ardhi, Mirathi, Vitambulisho vya NIDA, ZANID na vyeti vya kuzaliwa, jambo hilo linapaswa kutolewa elimu kwa wananchi.
Hata hivyo alisema wananchi waliowanyonge ndio wanaokumbana na kadhi hizo, huku wakishindwa kwenda kwenye vyombo vya sheria kutokana na kukosa uwezo, hivyo uwepo wa kampeni hiyo itawasaidia wananchi.
Mkuu huyo aliwasisitiza wataalamu hao kwenda kuwasikilisha wananchi wa makundi yote bila ya kujali jinsia, ulemavu na mambo mengine, lengo ni kuwapatia elimu hiyo ya msaada wa kisheria.
“Yapo makundi ya wajane, walemavu, Vijana, wazee, hata wafanyabiasra nendeni mukawapatie hiyo elimu ili waweze kujua haki zao,”alisema.
Katika hatua nyengine alisema elimu inahitajika na itaondoa changamoto zilizoko Vijijini, na kuweza kushajihisha kuleta amani katika nchi.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Mgeni Khatib Yahya alisema ujio wa kampeni hiyo utaleta faraja kwa wananchi, kwani changamoto zipo nyingi na wananchi wahajuwi wapi pakupata haki zao.
Aidha Mkuu huyo aliahidi Wilaya yake itashirikiana bega kwa bega na wataalamu hao, ili kuona wananchi wote wa Wilaya hiyo wanapata haki zao za kisheria.
Kwa upande wake Makurugenzi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Chake Chake Maulidi Mwalimu Ali, alisema zipo haki nyengine ambazo jamii inazihitaji, ikiwemo kupatiwa elimu juu ya suala la mirathi, ardhi na talaka.
Aidha aliwashauri wanakamati hao, kuhakikisha wanawafikiwa wananchi walioko kwenye madiko, sokoni, vijiwe vya boda boda, bajaji, hata shehia ya Ndagoni, Kibokoni na Uwandani ambapo changamoto ziko nyingi huko.
Nae mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Kusini Pemba, Bakari Omar Ali aliwashukuru viongozi hao kwa kuwapamoja nao wakati wote wa maandalizi ya kampeni hiyo, pamoja na kuahidi watatoa huduma ya Msaada wa kisheria ipasavyo kwa wananchi.
Alisema kampeni hiyo ni siku tisa kwa mkoa wa kusini Pemba, watahakikisha wanafika katika maeneo yote, ikiwemo katika visiwa vidogo vidogo.
Nae mratib wa kamepeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Wilaya ya Chake Chake Salama Suleiman Abdullah, alisema wataalamu wamejipanga vizuri kutoa elimu kwa wananchi wote katika shehia zao.
Nae mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanashenia Mkuu Pemba Safia Saleh Sultani, alisema mashirikiano ndio kitu Pekee kitakacho weza kuwasaidia kufikia malengo ya kampeni hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanapata elimu.
Kwa upande wa skuli ambazo zimepatiwa elimu ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa siku ya kwanza ni Madungu Msingi, Michakeeni Msingi na Skuli ya Chanjaani Msingi.