TEHAMA ni nyenzo muhimu katika sekta ya elimu, kwa kutambua hilo Serikali imewezesha mafunzo kwa walimu ili kuongeza maarifa na kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji ngazi mbalimbali za elimu.
Ameeleza hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Aprili 06, 2025 akizungumza na Clouds TV kuhusu maandalizi ya Kongamano la eLearning Africa 2025 kuanzia tarehe 7 hadi 9 Mei, 2025 JNICC jijini Dar es Salaam.
‘’matumizi ya TEHAMA yanatumika kikamilifu katika sekta ya elimu, walimu wote wamefundishwa namna ya kutumia teknolojia katika kufundisha, lengo letu ni kuhakikisha wana maarifa na mbinu za kidijiti zinazochagiza ujifunzaji’’ Alisema Prof. Nombo.
Amesema kongamano hilo linatoa fursa mbalimbali kwa nchi, ikiwa ni pamoja na maonesho ya bunifu na teknolojia zikiwemo zilizobuniwa na vijana wa kitanzania zinazolenga kutoa suluhu za kidijiti na kielimu.