Dar es Salaam, Mei 15, 2025 – Airtel Tanzania imezindua maduka mapya matano ya huduma kwa wateja katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, kwa lengo la kuimarisha utoaji huduma kwa wateja wake na kuongeza upatikanaji wa huduma hizo kwa mamilioni ya watanzania.
Maduka hayo yanayopatikana Sinza, Mikocheni, Mwananyamala na Magomeni, ni sehemu ya mkakati wa Airtel wa kusogeza huduma za muhimu kwa wateja wake wanaozidi milioni 20. Uzinduzi huo ulifanyika rasmi Sinza kwenye moja ya maduka hayo mapya na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adrianna Lyamba.
“Kwa kuzindua maduka haya, tunahakikisha kila mteja wa Airtel Tanzania anapata huduma za uhakika na haraka popote atakapokuwa,” alisema Adrianna Lyamba, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto.
“Kila moja ya maduka haya yamewekwa kimkakati kulingana na mrejesho wa wateja na uhitaji wa huduma ili kujenga urahisi na ubora wa huduma kwenye Jamii.
Kuongezwa kwa maduka haya ya huduma kwa wateja, Airtel sasa imepanua uwanda wake kwa kutoa huduma nyingi zaidi ikiwemo;
Kujisajili na kubadili laini za simu
Huduma za Airtel Money kwa wateja na mawakala
Mauzo ya vifaa vya Home Broadband kwa ajili ya intaneti majumbani ikiwemo router za 5G na MiFi
Kubadilisha nywila ya Airtel Money na kurejesha akaunti
Mauzo ya simu janja na vifaa vingine
Huduma nyingine kwa ajili ya wateja
Lyamba pia alisisitiza kuwa maduka hayo mapya yatakuwa ni sehemu salama kwa ajili ya wateja ambao wanawasiwasi na utapeli kwasababu timu ya watoa huduma itakuwepo kuwasaidia, kuwaelekeza na kuwawezesha kujilinda na kuhakiki taarifa zao. Mpango huu unaunga mkono kampeni ya serikali ya #Sitapeliki ambayo inaendelea ili kutokomeza utapeli.
“Lengo letu ni kuhakikisha kila mtanzania anaweza kushiriki Uchumi wa kidijitali akiwa salama bila hofu ya vitisho vinavyotoka kwa matapeli wa mtandao. Maduka haya sii vituo vya huduma peke yako, bali ni vituo vya fursa, uzalishaji na ujumuishwaji.”
Maduka hayo mapya ya huduma kwa wateja yamejengwa kwa muundo ambao unaendana na uvumbuzi wa kidijitali na mazingira rafiki ili kutoa huduma suluhishi za haraka, na kuwapa wateja mwongozo sahihi.
“Tumeitafakari upya safari ya mteja kwa kutoa huduma ambazo ni za kibinadamu na za teknolojia ya hali ya juu. Maduka haya yamejengwa kupunguza muda wa mteja kusubiri kuhudumiwa, kupunguza umbali wa kufata huduma na kuwafikia wateja mahali walipo,” alieleza Lyamba.
Upanuzi huu wa hivi karibuni unaweka msisitizo kuhusu dhamira ya Airtel Tanzania kutoa huduma bora yenye viwango vya kimataifa ikienda sambamba na misingi ya upatikanaji, unafuu na uvumbuzi.